Jumuiya za EAC na SADC zatoa wito wa amani mashariki mwa DRC
9 Februari 2025Matangazo
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC walimaliza mkutano wa kilele wa kutafuta suluhisho la mgogoro wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kutaka usitishaji wa mara moja wa mapigano, kati ya serikali ya Kongo na kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda.
Rais wa Rwanda ambaye nchi yake inatajwa kuwaunga mkono waasi wa M23 alishiriki moja kwa moja kwenye mkutano huo, huku rais wa Kongo Felix Tshisekedi akihudhuria kwa njia ya mtandao.