Jumuiya za EAC na SADC kuujadili mzozo wa mashariki mwa DRC
1 Agosti 2025Matangazo
Mkutano huo kati ya EAC na SADC umelenga kuratibu juhudi za pamoja za kisiasa na kuimarisha mazungumzo ya kumaliza mapigano yanayoendelea katika maeneo ya Kivu.
Jopo jipya la wapatanishi limeundwa, likijumuisha marais wa zamani kutoka Ethiopia, Kenya, Nigeria, Afrika Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Viongozi hao wamesisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitaji mshikamano wa kikanda na nia ya kweli kutoka pande zote.