MigogoroKimataifa
Jumuiya ya SCO yalaani vikali vitendo vya Israel huko Gaza
1 Septemba 2025Matangazo
Taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la China, Xinhua, wanachama hao 10 wa SCO pia wameikosoa vikali Marekani na Israel kwa kuishambulia Iran mnamo mwezi Juni. Taarifa hiyo imetolewa baada ya mkutano wa kilele wa SCO katika mji wa Tianjin, China.
Imeongeza kuwa mataifa wanachama wana wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa mzozo kati ya Israel na Palestina na kutoa wito wa usitishwaji wa kudumu wa mapigano na ufikishwaji usio na vikwazo wa misaada ya kibinadamu.
Mapema Jumatatu, Jumuiya ya Kimataifa ya wasomi wa masuala ya mauaji ya kimbari ilipitisha azimio linalosema kwamba vigezo vya kisheria vinathibitisha Israel inafanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.