Julia Klöckner achaguliwa Spika wa Bunge la Ujerumani
25 Machi 2025Bunge hilo jipya linatarajiwa kushuhudia kile kinachoweza kuwa kipindi cha mvutano baada ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kinachopinga uhamiaji kushikilia karibu robo ya viti vya bunge hilo kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita.
Spika Klöckner, mwenye umri wa miaka 52, amechaguliwa kwa kura 382 dhidi ya 204, huku wabunge 31 wakikosa kushiriki kura hiyo.
Klöckner aliwaahidi wabunge hao kwamba atatekeleza majukumu yake bila mapendeleo, kwa utulivu na ujasiri.
Bado haijabainika ni lini bunge hilo litaweza kumteuwa kansela mpya.
Spika huyo mpya, ameongeza kuwa kuna kipimo cha wazi kwake ambacho ni nidhamu na kwamba lazima kuwe na hali ya kuvumiliana kwenye mijadala yenye utata kulingana na sheria wazi.
Bado haijabainika ni lini bunge hilo litamchagua kansela mpya kwasababu bado Kansela mtarajiwa Friedrich Merz yuko katika mazungumzo ya kuunda serikali na chama cha Social Democratic SPD cha Kansela anayeondoka Olaf Scholz.