JangaSudan
Uokoaji waendelea Sudan baada ya maporomoko ya udongo
2 Septemba 2025Matangazo
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumapili ya Agosti 31 katika kijiji cha Tarasin katika milima ya Marrah baada ya siku kadhaa za mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Darfur, magharibi mwa Sudan .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vikosi vya Ukombozi wa Sudan (SLM/A) vinavyodhibiti eneo hilo, kijiji kilichoathirika kimezama kabisa ardhini na juhudi za uokoaji zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na hali ya kijiografia na ukosefu wa vifaa.
Wito umetolewa kwa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa kuingilia kati haraka ili kusaidia katika kuitoa miili ya wahanga. Umoja wa Afrika umezitaka pande zinazozozana nchini Sudan kusitisha mapigano na kuungana katika kutoa msaada kwa waathiriwa.