Juhudi za kutafuta manusura zaidi Afghanistan zaendelea
3 Septemba 2025Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Taliban, Zabihullah Mujahid, takwimu hizo zinahusu jimbo la Kunar pekee.
Tetemeko hilo, lenye ukubwa wa 6.0 katika kipimo cha Richter, lilitokea usiku wa Jumapili na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Nyumba nyingi zilizojengwa kwa matofali ya udongo na mbao ziliharibika huku baadhi ya wakaazi wakifukiwa chini ya vifusi.
Eneo hilo la milimani linaendelea kuwa changamoto kwa juhudi za uokoaji na usambazaji wa misaada, hali iliyolazimu mamlaka kutuma makomando kwa njia ya anga ili kuwafikia waathiriwa katika maeneo ambayo helikopta haziwezi kutua.
Hilo ni tetemeko la tatu kubwa tangu Taliban waingie madarakani mwaka 2021, na limetokea wakati nchi hiyo bado inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, uhaba wa misaada ya kifedha na changamoto za kibinadamu kutokana na na mamilioni ya wakimbizi waliorejeshwa kwa nguvu kutoka Iran na Pakistan.