JUBA:Majadiliano ya amani ya Uganda yameahirishwa
25 Julai 2006Matangazo
Mazungumzo ya amani yenye azma ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 19 kaskazini mwa Uganda yameahirishwa kwa juma moja. Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na waasi wa LRA yalianza tarehe 14 mwezi Julai mjini Juba.Naibu rais wa Sudan ya Kusini,Riek Machar alie mpatanishi katika mazungumzo hayo amesema maendeleo madogo yamepatikana na sasa wameahirisha mazungumzo hayo ili kuweza kushauriana.Afisa wa serikali ya Uganda amesema, ikiwa majadiliano ya amani hayatofanikiwa, serikali inaacha wazi uwezekano wa kuwashambulia waasi wa LRA nchini Kongo.Makamu waziri wa ulinzi wa Uganda,Ruth Nankabirwa amesema,Uganda ina wajibu wa kuwalinda wananchi wake na haiwezi kukaa na kutazama waasi wakijipanga upya nchini Kongo.