Burkardt ahamia Frankfurt kutokea Mainz
4 Julai 2025Gazeti la Bild la Ujerumani limripoto siku ya Ijumaa kwamba mshambuliaji wa timu ya Mainz 05 Jonathan Burkardt amekamilisha uhamisho kujiunga na timu ya Eintracht Frankfurt.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, klabu ya Frankfurt italipa ada ya uhamisho kiasi euro milioni 23 kwa kuwa Burkardt yuko chini ya mkataba na Mainz hadi mwaka 2027. Mchezaji huyo ametia saini mkataba na Frankfurt hadi Juni mwaka 2030.
Burkardt alikuwa mfungaji bora wa Bundesliga miongoni mwa wachezaji wengine raia wa Ujerumani akiwa na jumla ya magoli 18 katika mechi 29. Katika orodha jumla, alikuwa mfungaji bora nambari nne nyuma ya Harry Kane wa Bayen Munich, Patrick Schick wa Bayer Leverkusen na Serhou Guirassy wa Borussia Dortmund.
Oktoba mwaka 2024 Burkardt alicheza mechi yake ya kwanza na timu ya taifa ya Ujerumani.