Kufuatia uchaguzi wa bunge wa Jumapili ( 23.02.2025) nchini Ujerumani, Muungano wa kihafidhina wa CDU/CSU ulipata asilimia 28.5 ya kura, ukifuatiwa na AfD iliyojikingia asilimia 20.5 kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi. Seneta wa chama cha CDU katika jimbo la Berlin Joe Chialo, mwenye asili ya Tanzania amewashukuru wapigakura kwa kukipa ridhaa chama chao.