Jeshi la Uganda lawaua waasi 242 mashariki mwa Kongo
23 Machi 2025Wakati huo huo jeshi la uganda limesema lilifanikiwa kuwarejesha nyuma wanamgambo wa kundi la CODECO katika jimbo la Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Kongo, baada ya waasi hao kuwasahambulia wanajeshi wa Uganda katika mji wa Fataki.
Mwanajeshi mmoja wa Uganda aliuawa. Vyanzo vya ndani vimethibitisha kuwepo na mapigano. Tangu mwaka 2021, jeshi la Uganda lilipelekwa katika eneo la mashariki mwa Kongo kwa ajili ya kuzuia
kuenea kwa waasi wa Uganda wa ADF. Na wanamgambo wa Kongo wa CODECO wanadaiwa kuwa na mafungamano na wapiganaji wa ADF katika jimbo la Ituri.
Kundi la CODECO, ambalo liliibuka kutokana na mzozo wa kikabila kuhusu matumizi ya ardhi, linaongeza mashambulizi yake katika miezi ya hivi karibuni, kwa kuvichoma moto vijiji na uporaji huko jimboni Ituri.