Jeshi la Ukraine laongeza vikosi mashariki kuidhibiti Urusi
15 Agosti 2025Matangazo
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ametuma vikosi vya jeshi mashariki mwa nchi hiyo, ambako wanajeshi wa Urusi wamepiga hatua za haraka kuelekea katika eneo ambalo ni kitovu cha uchimbaji wa madini cha Dobropillia.
Akiandika kwenye mtandao wa kijamii,Zelensky amesema kwamba uamuzi huo umefanywa ili kuimarisha eneo hilo na maeneo mengine yaliyopo katika mkoa wa Donetsk.
Akizungumzia kuhusu mkutano wa kilele kati ya marais wa Marekani na Urusi kuhusu vita hivyo, Zelensky amesema huu ni muda wa kumaliza vita na kwamba Urusi lazima ichukue hatua zinazohitajika ili kufanikisha hilo.
Rais huyo ameweka wazi kwamba wanaitegemea Marekani na anatumai kwamba mkutano wa leo wa Trump na Putin utafanikisha mkutano wa pande tatu utakaoihusisha Ukraine.