Jeshi la Ukraine laahidi kuongeza mashambulizi Urusi
22 Juni 2025Matangazo
Syrsky amesisiza kuwa Ukraine haitasalia katika kujilinda pekee, badala yake inaendelea kushambulia ili kuepuka kupoteza watu na maeneo. Aidha Kamanda huyo alikiri kuwa Urusi ina faida katika matumizi ya ndege zisizo na rubani.
Hata hivyo Syrsky amesema Ukraine bado inadhibiti katika mkoa wa Kursk, kauli inayopingwa na Urusi. Kwa sasa, Urusi inadhibiti takriban robo ya Ukraine na imejitangaza kuwa mmiliki wa mikoa minne ya Ukraine tangu kuanzishwa kwa uvamizi mwaka 2022, pamoja na eneo la Crimea tangu mwaka 2014.
Ukraine inaishutumu Moscow kwa kuvuruga makubaliano ya amani ili kuendeleza vita na kuendelea kunyakua maeneo zaidi.