MigogoroAfrika
Jeshi Uganda kuimarisha ulinzi Mashariki mwa Kongo
31 Januari 2025Matangazo
Jeshi hilo limesema lengo la hatua hiyo ni kukataa na kuyazuia makundi mengine ya wapiganaji wenye silaha yanayofanya shughuli zake mashariki mwa Kongo kutumia vibaya hali ilivyo kwenye eneo hilo.
Uganda ina jukumu tata katika ukanda huo, ikiwa inashirikiana na vikosi vya Kongo katika Operesheni Shujaa dhidi ya kundi la Kiislamu la Allied Democratic Forces, linalohusishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.
Soma pia:Tshisekedi aidhinisha jeshi la Uganda kuingia Congo
Lakini pia inashutumiwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na wengineo, kuwaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya maslahi ya Kongo kwa kuwaruhusu kutumia eneo la Uganda kama njia ya usambazaji, ingawa Uganda inakana.