Jeshi la Sudan laukomboa uwanja wa ndege wa Khartoum
26 Machi 2025Chanzo cha kijeshi kimesema jeshi limechukua udhibiti kamili wa uwanja huo.
Baada ya kuikamata Ikulu ya Rais Ijumaa iliyopita, askari wameingia Khartoum, wakikamata majengo ya taasisi za serikali yaliyokamatwa na RSF tangu vita vilipoanza, kabla ya kuelekea kusini.
Afisa huyo ambaye hajataka kutajwa jina amasema kuwa kusini mwa katikati ya Khartoum, wanajeshi pia wamelizingira eneo la kimkakati la Jebel Awliya. Eneo hilo lilikuwa ngome ya mwisho kubwa ya RSF katika eneo la Khartoum, kutoka kaskazini, kusini na mashariki.
Tangu Aprili 2023, vita hivyo vimewauwa maelfu ya watu, na kuwaacha wengine zaidi ya milioni 12 bila makazi.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni 3.5 walilazimika kukimbia mji mkuu, na kuvitelekeza vitongoji vyote.