Jeshi la Sudan laukomboa uwanja wa ndege kutoka kwa RSF
26 Machi 2025Hilo ni tukio jingine muhimu katika mgogoro wa vita unaoendelea kati ya jeshi la wanamgambo wa RSF. Uwanja huo wa ndege ulikuwa mikononi mwa RSF.
Wakati hayo yakijiri, kiasi ya watu 61 wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Sudan kwenye soko moja la jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.
Shambulizi hilo limeharibu sehemu kubwa ya soko hilo la kila wiki la Tora lililoko umbali wa kilomita 80 kaskazini mwa el-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.
Kundi linalojulikana kama Darfur Network for Human Rights limesema shambulizi hilo lilitokea wakati soko hilo likiwa na shughuli nyingi na kufurika wanawake, watoto na wazee. Limesema watu wengine wengi walijeruhiwa katika shambulizi hilo la Tora.
RSF wanaendelea kudhibiti eneo la magharibi mwa nchi, na hasa Darfur, ambako wanataka kuanzisha serikali yao pamoja na washirika.