Jeshi la Pakistan lawauwa wanamgambo 54
27 Aprili 2025Katika taarifa, kitengo cha habari cha jeshi hilo, kimesema kuwa takriban wanamgambo 54 waliojaribu kuingia katika wilaya ya Waziristan Kaskazini kutoka Afghanistan waliuawa.
Baadhi ya abiria waliochukuliwa mateka wauwawa Pakistan
Taarifa hiyo imeongeza kuwa ripoti za ujasusi zinaashiria kuwa kundi hilo la wanamgambo lilikuwa linajipenyeza kwa amri ya wale walioitwa "mabwana wao wa kigeni" kufanya ugaidi ndani ya Pakistan.
Mzozo wazidi kufukuta kati ya India na Pakistan baada ya shambulio Kashmir
Jeshi hilo pia limedai kuwa jaribio la wanamgambo hao ni hatua inayoungwa mkono na mpinzani wake mkuu India.
Hapo jana, wanajeshi wawili wa Pakistan waliuawa wakati wa operesheni dhidi ya wanamgambo katika mkoa huo huo, ambao katika siku za nyuma umetumika kama ngome ya wapiganaji wa itikadi kali wanaohusishwa na mtandao wa Al-Qaeda pamoja na kundi la Taliban la Afghanistan.