UgaidiNigeria
Jeshi la anga la Nigeria lauua magaidi 35 wa Boko Haram
24 Agosti 2025Matangazo
Ehimen Ejodame, msemaji wa Jeshi la Anga la Nigeria amesema mashambulizi hayo yalilenga majimbo manne ya Kumshe, Borno, Katsina na karibu na mpaka wa Cameroon ambayo yamewezesha pia kuokolewa kwa mateka 76 wakiwemo wanawake na watoto.
Boko Haram, ni kundi la wapiganaji wenye itikadi kali huko nchini Nigeria na linazingatiwa kuwa moja ya makundi hatari zaidi ulimwenguni. Serikali ya Nigeria imekuwa ikijaribu kukabiliana na vurugu za makundi mbalimbali yenye silaha.