Jeshi la Israel limepata miili ya mateka watatu Gaza
22 Juni 2025Matangazo
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel imedokeza kwamba miili hio iliyopatika katika operesheni maalum ni ya mateka Ofra Keidar, Yonatan Samerano na Sajenti Shay Levinson.
Kati ya mateka 251 waliotekwa wakati wa shambulizi la Oktoba mwaka 2023, 49 kati yao bado wanashikiliwa Gaza, wakiwemo 27 ambao jeshi la Israel linasema wamekufa.
Kampeni ya kijeshi ya kulipiza kisasi iliyoanzishwa na Israel imesababisha vifo vya takriban watu 55,908, wengi wao wakiwa raia, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza katika eneo linaloongozwa na Hamas. Umoja wa Mataifa unazichukulia takwimu hizi kuwa za kuaminika.