Jeshi la Israel layashambulia maeneo ya Hezbolah Lebanon
7 Agosti 2025Matangazo
Jeshi la Israel limesema limeyashambulia maeneo kadhaa ya Hezbollah kusini mwa Lebanon yakiwemo maghala ya silaha, maeneo ya kuvurumishia maroketi na maeneo yanayotumiwa kuhifadhi vifaa vya kiufundi.
Vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kuhusu mashambulizi ya kutokea angani ya Israel katika eneo hilo mapema hapo jana.
Mashambulizi hayo yamefanywa licha ya makubaliano wa kusitisha mapigano ambayo yamekuwa yakitekelezwa kati ya Israel na kundi hilo linaloungwa mkono na Iran tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka uliopita.
Ingawa mkataba huo bado upo rasmi, Israel inaendelea kufanya mashambulizi ya kila siku dhidi ya maeneo ya Hezbollah, ikitaka kundi hilo lipokonywe kabisa silaha.