Wapalestina wafukuzwa kaskazini mwa Gaza
22 Mei 2025Jeshi la Israel limetoa onyo la kuwataka wapalestina kwenye maeneo 14 ya Kaskazini mwa Gaza waondoke, huku likiendeleza operesheni yake mpya ya mashambulio inayokosolewa na kulaaniwa kimataifa.
Onyo hilo limetolewa saa chache baada ya Umoja wa Mataifa kusema umekusanya na kuanza kusambaza misaada iliyoingizwa Gaza na malori 90. Msaada huo ni wa kwanza kuingia kwenye eneo hilo tangu Israel ilipoweka vizuizi kila mahali kwenye Ukanda huo tarehe 2 mwezi March.
Jens Laerke, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kiutu,OCHA amesema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kusambaza msaada huo kutokana na ukosefu wa usalama,kitisho cha uporaji na kukosekana ushirikiano na maafisa waIsrael.
Jeshi la Israel limesema linaendesha operesheni kwenye maeneo 14 ya kaskazini mwa Gaza ambako limedai wanamgambo wa Hamas wanaendesha shughuli zao.