Jeshi la Israel lauwa 12 Gaza
28 Julai 2025Matangazo
Mashambulizi hayo ya anga ya usiku wa kuamkia Jumatatu (Julai 28) kwenye kitongoji cha Khan Younis yanafanyika wakati jeshi la Israel limetangaza kile linachokiita 'usitishaji mashambulizi wa kimkakati' kwenye baadhi ya maeneo ya Gaza kwa masaa kumi kwa siku ili kuruhusu misaada ya kibinaadamukuwafikia raia.
Hatua hiyo ya Israel inatokana na shinikizo kubwa la kimataifa na ukosoaji dhidi yake kwa jinsi inavyoendesha vita vyake kwenye Ukanda huo.
Jeshi hilo limedai usitishaji huo mashambulizi unahusu kwenye maeneo ambayo vikosi vyake haviko, kama vile al-Mawasi, Deir Balah, katikati ya Gaza na kaskazini mwa Gaza City.