Jeshi la Israel latambua kombora lililorushwa kutokea Yemen
4 Septemba 2025Matangazo
Jeshi la Israel limesema kombora lilivurumishwa kutokea nchini Yemen kuelekea Israel lilianguka katika eneo lililo wazi nje ya himaya ya Israel na hakuna ving'ora vilivyowashwa.
Waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz ameapa leo kuwalaani waasi wa Houthi wa Yemen na mapigo kumi ya kumi ya Biblia ya Misri baada ya waasi hao kuimarisha mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel.
Wahouthi wameapa kuongeza mashambulizi yao dhidi ya Israel baada ya waziri wao mkuu na maafisa wengine wa vyeo vya juu kuuliwa katika mashambulizi ya kutokea angani ya Israel wiki iliyopita.