JERUSALEM: Waandamanaji wamaliza maandamano yao nchini Israel
21 Julai 2005Matangazo
Waandamanaji wanaoupinga mpango wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza wamemaliza maandamano yao kwa wakati huu. Polisi nchini israel waliwazuia nmaelfu ya waandamanaji kusini mwa nchi hiyo waliotaka kuandamana katika mkanda wa Gaza.
Kiongozi wa baraza la wakaazi wa Gaza na ukingo wa magharibi, aliyeyapanga maandamanao hayo amesema watafikiria njia nyengine ya kuuzuia mpango huo wa kuyaondoa makazi yao.
Katika hatua nyengine ya kujaribu kuuzuia mpango huo, iliyoshindwa kufaulu, bunge la Israel limepiga kura kupinga kucheleweshwa kwa mpango wa kuyaondoa makazi 21 ya wayahudi kutoka Gaza na makazi manne kati ya 120 ya ukingo wa magharibi, unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.