JERUSALEM: Polisi wa Kimisri mpakani Gaza
1 Septemba 2005Matangazo
Bunge la Israel limeidhinisha makubaliano ya kuvidhibiti vikosi vya usalama vya Misri,eneo la mpakani kati ya Gaza na Misri,pale Israel itakapo ondoka kutoka eneo hilo.Makubaliano hayo yanatoa ruhusa ya kuwaweka polisi 750 wa Kimsri upande wa pili wa mpaka wa Gaza.Polisi hao wa mpakani watachukua nafasi ya vikosi vya Kiisraeli vilivyokuwepo huko tangu Israel kulikalia eneo hilo miaka 38 ya nyuma wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967.